28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Azam yaifuata KMC nusu fainali FA

Lulu Ringo, Dar es Salaam

Timu ya Azam FC, imefuzu katika hatua ya nusu fainali ya kombe
Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) baada ya kuichapa Timu ya Kagera Sugar goli 1-0 katika mchezo uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Goli hilo lilifungwa dakika ya 78 na Joseph Mahundi baada ya timu hizo kushambuliana kwa muda mrefu bila mafanikio yoyote.

Azam itakutana na Timu ya KMC kutoka Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam katika mchezo wa nusu fainali ambapo timu hiyo ilishafuzu hatua ya nusu fainali baada kuichapa timu ya African Lyon goli 2-0 katika mchezo uliochezwa Machi 28 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamhuyo jijini Dar es Salaam.

Mchezo wa Yanga SC dhidi ya Alliance FC utakaochezwa kesho jijini Mwanza ndiyo utakaoamua nani atavaana na Timu ya Lipuli FC kutoka mkoani Iringa ambayo imetinga hatua ya nusu fainali baada ya kuisweka Singida United ya mkoani Singida goli 1-0 katika mchezo uliochezwa juzi Machi 28, kwenye Uwanja wa Samora mkoani humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,455FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles