Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Mchezaji wa Yanga, Yannick Bangala raia wa DR Congo, amesaini mkataba wa miaka miwili Azam FC baada ya klabu hiyo kufikia makubaliano yakumnunua kutoka Jangwani.
Bangala ambaye ametambulishwa leo, Julai 29, 2023 na Azam, anakuwa mchezaji wa pili kutoka Yanga kujiunga na timu hiyo baada ya Feisal Salum.