Azam wamlilia mke wa Agrey Moris

0
1075

NA JESSCA NANGAWE-DAR ES SALAAM

UONGOZI wa Klabu ya Azam, umesema utakua bega kwa bega na familia ya nahodha wao, Agrey Morris ambaye amefiwa na mkewe akiwa kwenye harakati za kujifungua.

Mke wa Morris anayejulikana kwa jina la Asteria, alifariki usiku wa kuamkia jana akiwa hospitali alipokwenda kwa ajili ya kujifungua.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo,  Abdulkarim Amin ‘Popat’,  alisema wamepokea kwa masikitiko taarifa ya msiba huo na kuahidi kuwa karibu na mchezaji wao huyo kipindi hiki kigumu.

“Tunatoa salamu zetu za pole kwenda kwa familia ya Moris, pamoja na ndugu, jamaa na marafiki na wote walioguswa na msiba huu, Azam tunaungana na familia ya marehemu na tunamuomba Mwenyezi Mungu, awajalie nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu,”alisema Popat.

Alisema kulingana na taarifa waliyopewa na familia ya Agrey, mazishi ya marehemu Asteria yanatarajia kufanyika kesho kwenye makaburi ya Nyantila yaliyoko Kitunda jJijini Dar es salaam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here