23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, August 14, 2022

Azam wajipanga upya

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba, amewapa mapumziko ya siku tatu wachezaji wake, mara baada ya kumaliza mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa juzi Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Azam juzi walibanwa kwenye Uwanja wao wa nyumbani na kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya JKT Tanzania.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Kocha msaidizi wa Azam, Idd Nassor ‘Cheche’, alisema wanahitaji muda mrefu wa kuweka miili sawa kabla ligi haijaendelea.

“Tumepata sare ya mabao 2-2 dhidi ya JKT Tanzania, mchezo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa, kwani walitutangulia lakini tuliweza kurudisha mabao hayo na kutoka sare,” alisema.

Alisema baada ya mapumziko ya siku tatu kumalizika wataanza mazoezi kwa kuyafanyia kazi baadhi ya kasoro walizoziona katika mechi walizocheza.

Cheche alisema wanahitaji kuwa imara zaidi na kueleta ushindani katika mechi zao ili waendelee kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi.

Wakati huo huo mchezaji wa timu hiyo Frank Domayo ‘Chumvi’, aliondoka nchini alfajiri ya jana kuelekea jijini Cape Town, Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu ya tatizo la kuchanika msuli wa nyama ya paja ya mguu wa kulia. Domayo alipata maheraha hayo, wakati akiwa kwenye kambi ya timu ya Taifa, iliyokuwa ikijiandaa na mchezo wa kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2021 nchini Cameroon dhidi ya Guinea ya Ikweta.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,712FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles