22.9 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

Azam media yazindua tamthilia nne kwa mpigo

BEATRICE KAIZA

Kampuni ya Azam media imezindua filamu nne kwa mpigo zitakazokuwa zikionywesha kwenye chaneli ya sinema zetu kupitia kin’gamuzi cha Azam kuanzia Julai 13 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi huo, Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo, Tido Mhando amesema sasa ni wakati wa kuwapa burudani za kinyumbani zaidi watazamaji wao.

“Tumekuwa tukipokea malalamiko, maoni na ujumbe kutoka kwa watazamaji wetu kupitia mitandaoni wakitaka kuona tamthilia za kinyumbani na kuona wasanii kutoka hapa nchini hivyo tukaona kuna haja ya kuwaletea kitu wanachotaka na ndio maana tumeamua kuleta tamthilia nne kwa mpigo zilizotengenezwa na kuchezwa na watu maarufu, wakongwe na wapya kwenye tasnia hiyo,”

Amezitaja tamthilia hizo ni pamoja na panguso ya Jimmy Mafufu, single mama ya Jacob Steven ‘JB’, shilingi ya madebe Lidai na tandi ya Vicent kigosi ‘Ray’ zitakazoanza.

Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko, Sabrina Mohammed akuwa tamthilia hizo zitarushwa kwa kifurushi cha chini kabisa kuanzia  3,000 hadi 10000.

Kwa upande wake msanii mkongwe ambae pia ni mmoja wa waandaji wa tamthilia ya “single mama” Single Mtambarike amesema ni wakati wa kuifufua tasnia ya filamu na kuleta mapinduzi ya kiburudani zaidi.

“Bado tunaona mchango wa kuendelea kuwepo kwa wadau kama azam tv na wengine ni wazi tasnia inahitaji kufika mbali na kufikia soko la kimataifa,” amesema Mtambalike.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,429FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles