23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Azam Media yamwaga mamilioni Ligi Kuu

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Kampuni ya Azam Media imeingia makubaliano na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Bodi ya Ligi ya kurusha matangazo ya mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mkataba wa miaka 10 wenye thamani ya Sh bilioni 225.6.

Makubaliano hayo yameingiwa leo katika hafla iliyofanyika leo, jijini Dar es Salaam na mkataba huo mpya unatarajia kuanza kazi msimu ujao wa 2021/2022.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media, Tido Mhando, amesema thamani ya mkataba huo imetokana na uzoefu wa miaka minane katika kurusha matangazo ya mechi za Ligi Kuu ambako wamejifunza mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuona jinsi timu zinavyojiendesha na changamoto zake.

Tido amesema thamani ya mkataba huo ni kwa ajili ya maendeleo ya Ligi Kuu na kwa kutambua hilo, fedha ambayo imewekezwa , asilimia 67 itakwenda moja kwa moja kwa timu ambazo zinashiriki ligi hiyo.

Ameeleza kuwa msimu ujao wa 2021/2022, Azam Media itatoa Sh bilioni 12, huku timu zinazoshiriki katika Ligi Kuu zikipata bilioni nane, mgao mwingine utakwenda kwa maendeleo ya soka, TFF na Bodi ya Ligi Kuu (TPLB).

“Mfano kwa misimu mitatu ijayo yaani 2021/22 mpaka 2023/24, bingwa wa Tanzania Bara atakuwa akipata Sh milioni 500 kwa msimu. Mshindi wa pili milioni 250, mshindi wa tatu milioni 225 na mshindi wa nne milioni 200,”amesema Mhando.

Amesema fedha hizo, zitakuwa zikiongezeka kila msimu na msimu wa 2028/29 mpaka 2030/31 bingwa atakuwa akipata Sh milioni 700 kwa msimu, mshindi wa pili milioni 325, mshindi wa tatu milioni 275 na mshindi wa nne milioni 250.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles