27.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Azam kuweka kambi nje ya nchi

azam fcNA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

KLABU ya soka ya Azam FC, inatarajia kuweka kambi ya wiki moja nje ya nchi ili kujiandaa na mchezo wa mzunguko wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Bidvest Wits ya Afrika Kusini.

Azam itakutana na wapinzani wao Machi 12 kwenye Uwanja wa Bidvest jijini Johannesburg, kabla ya kurudiana Uwanja wa Azam Complex Machi 20 mwaka huu.

Akizungumza na MTANZANIA, Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Saad Kawemba, alisema kambi hiyo maalumu wataiweka kwenye nchi jirani na Afrika Kusini na kuondoka siku moja kabla ya mchezo huo kuingia Johannesburg.

“Tulipata nafasi ya kwenda jijini Ndola (Zambia), ili kujiandaa na michezo ya kimataifa pia kocha ameshaweka programu yake na tayari utawala umeshaifanyia kazi.

“Hata hivyo, timu yetu ipo tayari kwa maandalizi ya mchezo huo, tutaondoka baada ya kumaliza mchezo wetu  wa Ligi Kuu dhidi ya Yanga,” alisema Kawemba.

Kawemba aliongeza kuwa baada ya mchezo huo watarajea kwenye nchi waliyoweka kambi kuendelea na maandalizi na watatua jijini Dar es Salaam siku moja kabla ya mchezo wao wa kiporo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Stand United, utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex Machi 16, mwaka huu.

Endapo Azam ikifanikiwa kuvuka  kwenye mzunguko huo na kuingia mzunguko wa pili, itakutana na moja ya timu tatu kati ya Esperance de Tunis ya Tunisia au Renaissance FC ya Chad na New Star de Douala ya Cameroon, ambazo zinachuana raundi ya awali.

Esperance inasubiria kucheza na moja ya timu hizo kati ya Renaissance na New Star de Douala katika raundi ya kwanza kabla ya kukutana na Azam FC au Bidvest Wits kwenye raundi ya pili itakayoanza Aprili mwaka huu.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles