Azaki kuzindua Ilani uchaguzi serikali za mitaa

0
823

Asha Bani-Dar es Salaam

Asasi za Kiraia nchini (AZAKI), kesho wanatarajia kuzindua Ilani yao ya uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mwaka 2019 na uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Mkurugenzi Mkuu wa kituo cha taarifa kwa wananchi, Deus Kibamba amesema Ilani hiyo ni ya pili huku ya kwanza ilikuwa mwaka 2015 ambayo waliitumia katika kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala mbalimbali ya chaguzi.

Kibamba amesema katika kuhakikisha kuwa wananchi wànaweza kubainisha vipaumbele vya uchaguzi katika chaguzi za mwaka 2019 na 2020 Azaki walifanya tathimi ya kila ilani yao ya 2015 na baadae kuandaa mpya.

“Lengo kuu ya Ilani ya Azaki ya uchaguzi ni kuwasaidia watanzania kubainisha vipaumbele vikuu watavyotumia kuchagua viongozi wenye uwezo wa kuvitekeleza na kuweka vipaumbele hivyo vya watanzania katika lugha rahisi kwa ajili ya kushawishi wagombea na vyama kuvibeba kama agenda zao kabla na baada ya uchaguzi ,”amesema Kibamba.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here