27 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

Azaki 200 zaandika andiko kupambana na corona

Avelyn Kitomari-Dar es Salaam

ZAIDI ya Asasi za Kiraia  (AZAKI) 200 kutoka maeneo yote nchini zimeshiriki  kuandaa andiko la namna ya kupambana na maambukizi ya virusi vya corona  lengo likiwa ni  kuongeza ufanisi wa kukabiliana na janga hilo.

Mratibu wa Kitaifa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa alisema  wameandaa mpango huo kwa kufanya  tathmini na kuainisha changamoto zilizojitokeza.

“Pia  tumeangalia  madhara mbalimbali yaliyotokea na kuona ni kwa jinsi gani wanaweza kuwa sehemu ya kuendeleza hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kupambana na janga hili.

“Katika mpango mkakati wetu maeneo ambayo AZAKI  imepanga kushirikiana na Serikali ni pamoja na uhamasishaji juu ya hatua za kujikinga, utoaji wa huduma,ushauri na kusaidia pale changamoto zinapojitokeza, mikakati ya kupunguza matokeo hasi , pamoja na kuweka mpango wa pamoja baina ya Serikali na sisiI”,alisema.

Aliipongeza Serikali kwa hatua wanazochukuwa  kukabiliana na ugonjwa huo na kusema ipo haja ya kuunga mkono juhudi zinazochukuliwa.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Faustine Ndugulile  alisema Serikali itaendelea kushirikiana na AZAKI katika kupambana na maambukizi ya  corona. 

Alisema AZAKI pamoja na wananchi  wanao, wajibu wa kushirikiana na Serikali kupambana na ugonjwa huo, ambao ni janga la dunia lililoleta athari za kiuchumi na kiafya na kusabisha vifo vingi kwa muda mfupi.

 Mwenyekiti Shirikisho la Vyama la Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Ummy Nderiananga aliwashukuru wataalamu wa afya kwa huduma wanayoitoa kwa wananchi waliopata maambukizi ya ugonjwa huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,454FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles