AY: Wakongwe Bongo fleva hawataki kubadilika

0
956

3. AYNA HERIETH FAUSTINE

MSANII mkongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ambwene Yesaya, ‘AY’, amesema baadhi ya wasanii wakongwe wanashindwa kuendana na muziki wa sasa kwa kuwa hawataki kubadilika kama muziki huo unavyotaka.

Msanii huyo anayetamba na wimbo wa ‘Zigo Remix’, aliomshirikisha Diamond Platinum ambao umeamuliwa na TCRA kuchezwa usiku tu, alisema wasanii hao wanaendelea kubweteka na ushauri unaowataka wakomae katika aina ya muziki wanaofanya, wanasahau muziki umebadilika na unataka kubadilishwa kama unavyotaka.

“Maisha ya binadamu hayawezi kwenda bila kubadilika, wasanii wengi hawapendi kubadilika hata wakipewa ushauri wanapenda kubaki na yale yale bila kuendelea mbele, sisi tunaendelea kwa kuwa tunaufuata muziki unavyotaka,” alisema AY.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here