20.5 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Aweso ang’oa wawili kushindwa kusimamia miradi ya maji Pangani

Oscar Assenga -Pangani

NAIBU Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amemsimamisha kazi Meneja wa Wakala wa Usambazaji Maji Vijijini Wilaya ya Pangani (Ruwasa Pangani), Ladislaus Modestus.

Pia ameagiza Mkurugenzi wa Usambazaji wa Maji na Usafi wa Mazingira wa Ruwasa makao makuu, Mkama Bwire, kuondoka na meneja huyo kutokana na kushindwa kusimamia miradi, huku mingine akiwa haitambui.

Aliagiza pia Meneja wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Wilaya ya Pangani, Adam Sadick kusimamishwa kazi kutokana na kushindwa kusimamia miradi na bili za maji na kusababisha mamlaka kupata hasara.

Alisema mkurugenzi anapoondoka aondoke na mhandisi huyo ambayo ameshindwa kuendana na kasi ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji ambayo ni muhimu kwa ustawi wa maisha yao.

Alisema hatua hiyo, inatokana na mhandisi kupewa fedha za kusimamia mradi Sh milioni 26, lakini bado hafiki maeneo yanayotekelezwa miradi.

“Ndugu yangu, wewe ni mhandisi wa maji upo hivi, kama ungekwa daktari si ungekuta umekwishaua watu, hatuwezi kukubali kuona hali hii, hatupo tayari kuona watu wa namna hii

 “Kutokana na mhandisi unapata fedha za kusimamia miradi ya maji unashindwa kufanya, hata ukiangalia msafara wangu ameupoteza, wewe hautufai, bora uondoke naye,” alisema.

Kutokana na hali hiyo, aliagiza kuundwa tume itakayobaini nini changamoto iliyopo kwenye usimamizi wa miradi ya maji Pangani.

“Pia eneo la Kibinda lina changamoto kubwa ya maji, nilimfuata Waziri Kamwele (Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe) nikamwambia suala hilo… niambieni  mabomba yanafika lini?” alihoji.

 Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Zainabu Abdallah, alisema wananchi wanakabiliwa na changamoto ya maji zaidi ya wiki tatu.

Alisema alikuwa likizo, lakini alilazimika kurudi  na kwenda eneo la mradi kukagua maji, na aligundua changamoto tatu.

Moja ni mfumo wa umeme, pampu kuwa na uwezo mdogo kuliko inavyopaswa kutumika kwenye maji.

“Wataalamu wanasema pampu ina uwezo mdogo, mimi nashangaa wakati ikinunuliwa… mashine ya kuvuta umeme na kuzima mashine zipo mbili na moja ni mbovu na pampu zaidi ya milioni 22 ni mbovu, anasema maelezo ya mkandarasi mfumo wa umeme mbovu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,058FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles