23.8 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

AVRIL AKANUSHA KUFANYIWA UPASUAJI

NAIROBI, KENYA


BAADA ya staa wa muziki nchini Kenya, Avril Nyambura, kujifungua mtoto wa kwanza wiki iliyopita, taarifa zilisambaa kuwa mrembo huyo alipata tatizo wakati huo wa kujifungua kwa kawaida na hatimaye alifanyiwa upasuaji, lakini msanii huyo amekanusha.

Kwa mara ya kwanza msanii huyo ametumia ukurasa wake wa Instagram na kuzungumzia juu ya suala hilo, akisema: “Nimekuwa nikiona habari nyingi zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii juu ya kujifungua kwangu.

“Naomba niweke wazi kuwa habari hizo zote hazina ukweli kama vile kujifungua kwa upasuaji, lakini ukweli ni kwamba nilijifungua salama bila ya tatizo lolote kama watu wanavyodai.

“Hata hivyo, kulikuwa na taarifa kwamba nimepata mtoto wa kike, si kweli Mungu amenipa mtoto wa kiume, nawashukuru wote waliokuwa pamoja na mimi kwa kipindi hiki na mwanangu anaendelea vizuri,” alisema Avril.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles