22.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Aveva aanza na makundi Simba

NA ZAITUNI KIBWANA

Evans Aveva
Evans Aveva

, ameanza rasmi kazi hiyo kwa kupanga mkakati wa kuvunja makundi yote ndani ya timu hiyo ili Simba iwe moja.

Aveva aliyekuwa akipambana na Andrew Tupa kwenye nafasi hiyo na kufanikiwa kumbwaga kwa kishindo baada ya kupata kura 1,455 dhidi ya 388 za Tupa, alisema kuna haja ya kufanya hivyo.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwa Rais mpya na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Amini Bakhressa, Aveva alisema atavunja makundi yote kwa ajili ya kuijenga Simba.

Aveva ambaye ni mwanachama wa kundi la Friends of Simba, alisema makundi yaliyotokea kwenye harakati za uchaguzi huo hayana maana tena yavunjwe.

“Sioni sababu ya makundi hayo kuendelea, makundi yaliyokuwepo Simba kwa ajili ya uchaguzi tunayavunja kwa ajili ya kuiendeleza timu yetu kwa pamoja,” alisema.

Wakati Aveva akiyasema hayo, Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi aliyekaimu nafasi hiyo baada ya Damas Ndumbaro kuwa nje ya nchi, Amini Bakhressa alitoa ya moyoni baada ya kumuusia rais huyo kutoiacha Simba katika kipindi chote.

Bakhressa aliamua kutoa usia huo, baada ya Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Ismail Aden Rage na Kamati yake ya Utendaji iliyomaliza muda wake kuamua kuingia mitini kabla ya rais mpya hajapatikana.

“Uongozi ni kama vijiti tu watu hupokezana nawashangaa Rage na kamati yake kuamua  kuingia mitini kabla ya rais mpya hajapatikana wakati wao ndio walipasa kumtangaza mrithi wao,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles