30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Auto Solskjaer awajia juu wachezaji wake

MANCHESTER, ENGLAND

BAADA ya Manchester United kutolewa kwenye michuano ya Kombe la FA dhidi ya Wolves, kocha wa timu hiyo, Ole Gunnar Solskjaer, amewajia juu wachezaji wake kwa kitendo cha kucheza mfumo wa Jose Mourinho.

Manchester United ilikubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Wolves kwenye hatua ya robo fainali, ambayo ilipigwa kwenye uwanja wa Molineux na kuondolewa kwenye michuano hiyo.

Kwa mujibu wa The Sun, Solskjaer aliwashangaa wachezaji wake katika dakika 45 za kipindi cha kwanza na kuwataka wabadilike dakika za mwisho kwa ajili ya kupata matokeo, lakini walishindwa kufanya hivyo na kujikuta wakitolewa.

Hata hivyo, kocha huyo amewataka wachezaji wake kila mmoja kuhakisha anaeleza kwa nini walicheza chini ya kiwango.

Bila kujali Man United imesalia kwenye michuano mikubwa ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, anaamini walikuwa na nafasi kubwa ya kutwaa Kombe hilo la FA.

“Tumerudi hatua nyingi nyuma, naweza kusema kwamba United wameonesha kiwango cha chini sana tangu nimewasili hapa. Tulicheza vizuri katika mchezo dhidi ya Arsenal, lakini hatukupata kile tulichokitarajia.

“Nadhani wachezaji wangu walijisahau na kucheza mfumo ambao walikuwa wanautumia na kocha Jose Mourinho, lazima wabadilike na bila kufanya hivyo tunaweza kujikuta tunaelekea pabaya.

“Najua hauwezi kuwa kwenye kiwacho cha hali ya juu katika kila mchezo msimu wote, kuna wakati unakutana na changamoto mbalimbali,” alisema kocha huyo.

Kocha huyo aliongeza kwa kuwatoa wasiwasi mashabiki wa timu hiyo kuelekea michezo ijayo huku akidai wanaelekeza nguvu zao huko kwa ajili ya matokeo.

Mchezo unaofuata kwa Manchester United ni dhidi ya Watford mwishoni mwa mwezi huu, baada ya kupisha michezo ya Kimataifa wiki hii. United inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi ikiwa na pointi 58, baada ya kucheza michezo 30. Wakati huo Liverpool wakiwa vinara kwa pointi 76, wakifuatiwa na Man City wenye pointi 74, lakini Liverpool wanaongoza kwa mchezo mmoja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles