22.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Aussems ataka mvua ya mabao

THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amesema anahitaji ushindi wa mabao mengi katika kila mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Simba  inakabiliwa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting unaotarajiwa kuchezwa Novemba 24 mwaka huu, Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Wekundu hao wanakamata uongozi wa ligi hiyo, wakiwa na pointi 22, baada ya kushuka dimbani mara tisa, wakishinda michezo saba, sare moja na kuchapwa mara moja.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Aussems alisema bila ya kuangalia ni timu gani wanakutana nayo lazima wazidishe umakini katika kuhakikisha wanatoka kifua mbele ndani ya dakika 90 za michezo yao.

“Napenda kuona timu yangu ikipata matokeo ya mabao mengi katika kila mechi, yeyote yule afunge kwani endapo ukifanya makosa unaweza kujikuta umepoteza,” alisema.

Alisema hana mpango wa kucheza mchezo wa kirafiki na timu yoyote wakati huu wa mapumziko mafupi ya ligi kupisha michezo ya kimataifa ya timu za taifa.

“Labda  tutacheza mechi ya mazoezi na kikosi B siku ya Jumatatu ili kuendelea kuwaweka fiti wachezaji wangu,”alisema.

Aussems alisema kwa sasa wanaitazama michezo inayowakabili mbele yao ili waweze kufanya vizuri na kupata kile wanachokihitaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,526FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles