24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

Aua mkewe kwa panga kisha naye ajinyonga

Na DAMIAN MASYENENE -SHINYANGA

MKAZI wa Kijiji cha Igunda Wilaya ya Kipolisi Ushetu mkoani Shinyanga, John Chumila (42), anadaiwa kumuua mke wake, Christina Jacob (41) kwa kumkata na panga kichwani na shingoni kisha na yeye kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Joseph Paul alisema kuwa tukio hilo lilitokea Juni 21, mwaka huu saa 3 usiku nyumbani kwa marehemu hao huku chanzo ikidaiwa kuwa wivu wa mapenzi.

Alisema marehemu hao walikutwa chumbani na miili yao imekabidhiwa kwa ndugu kwa taratibu za mazishi.

Kutokana na kuendelea kuwepo kwa matukio ya mauaji yanayotokana na wivu wa kimapenzi, Kaimu Kamanda huyo wa Polisi, alitoa wito kwa wanandoa kuacha tabia za kujichukulia sheria mikononi, hivyo wafuate taratibu za kuwapeleka wenza wao kwenye madawati yaliyopo ofisi za ustawi wa jamii pamoja na vituo vya polisi ili kupata ufumbuzi pindi wapatapo matatizo katika ndoa zao.

Katika tukio lingine, jeshi hilo linafanya uchunguzi wa tukio la kujaribu kujiua lililotokea Juni 22, mwaka huu saa 12 jioni katika Kijiji cha Bugimbagu Manispaa ya Shinyanga, ambapo Malembeka Jisinza (50) akiwa nyumbani kwake alijikata sehemu zake zote za siri kwa kutumia kisu. Pia alijikata sehemu za tumbo juu ya kitovu.

Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na majeruhi huyo amelazwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga akiendelea na matibabu.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,249FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles