27.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Atupwa jela miaka 2 kwa kughushi vyeti vya uuguzi

Na TUNU NASSOR

-DAR ES SALAAM

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Pwani imemuhukumu kwenda jela miaka miwili Anna Kasanda kwa kosa la kughushi na kutumia vyeti bandia.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Rose Kangwa, alisema mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa utetezi kuwa mtuhumiwa alikuwa anatumia vyeti bandia.

“Mtuhumiwa anahukumiwa kwenda jela miaka miwili kwa kosa la kwanza la kughushi leseni ya uuguzi na ukunga kinyume cha kifungu cha sheria namba 355(a) na 337 cha mwaka 2002,” alisema Rose.

Alisema kwa kosa la kujaribu kuihuisha (renew) leseni hiyo, mtuhumiwa atatumikia miaka miwili mingine.  

Rose alisema japokuwa hakuna sehemu katika ushahidi inaonesha mtuhumiwa anamiliki mashine ya kuchapa nyaraka hizo, lakini kwa mujibu wa shahidi wa pili inaonesha kuwa mtuhumiwa alitaka kuendelea kutumia vyeti hivyo.

Akizungumza na MTANZANIA, Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC), Agness Mtawa, alisema wanalaani vikali matumizi ya leseni bandia za baraza hilo.

Alisema kwa kufanya hivyo inaweza kuleta madhara makubwa katika jamii kwa kuwa huenda muhusika akatumia leseni hiyo kutoa huduma ambayo hana taaluma nayo.

“Uuguzi ni taaluma inayotakiwa kusomea, kusajiliwa na kupewa kibali ndipo utoe huduma kwa wagonjwa, hivyo tunalaani kitendo hicho,” alisema Mtawa.

Aidha msajili huyo alitoa onyo kwa wote wenye tabia kama hizo kuacha mara moja kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na ni kuhatarisha afya za wanaohudumiwa.

“Nawaonya wanaofanya vitendo hivyo kuwa tutawatafuta popote walipo na kuwafikisha katika vyombo vya sheria,” alisema Mtawa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,903FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles