27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 4, 2023

Contact us: [email protected]

ATCL yasitisha safari za ndege Afrika Kusini

Asha Bani, Dar es Salaam

Siku moja baada ya Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), iliyokuwa inashikiliwa kwa amri ya Mahakama ya Gauteng nchini Afrika Kusini, kabla ya mahakama hiyo hiyo kuamuru iachiwe jana, imewasili nchini huku ikisitisha safari zake nchini humo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Septemba 5, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe ndege hiyo imetua nchini jana saa moja usiku lakini itasitisha safari zake za kwenda Afrika Kusini kwa sasa kutokana na  sababu mbalimbali ikiwamo vurugu zinazoendelea nchini humo.

“Sababu hizo ni pamoja na usalama wa chombo chenyewe kutokana na hali ya vurugu iliyopo nchini humo hadi pale tutakapohakikishiwa usalama wetu na abiria.

“Wanasheria wamebaki Afrika Kusini wakiendelea kufuatilia hukumu iliyotolewa na kuhakikisha aliyefungua kesi analipa gharama zote,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, amesema leo asubuhi ndege hiyo imefanyiwa ukaguzi iko salama inasubiri kupangiwa safari ya njia nyingine itakayoanza leo saa tisa alasiri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles