Askofu Shoo atuma salamu za rambirambi

0
1142

Na Safina Sarwatt- Kilimanjaro


MKUU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Fredrick Shoo, ametoa salamu za rambirambi kwa Watanzania wote katika kipindi hiki ambacho Taifa limekumbwa na majonzi kutokana na ajali ya kuzama kwa Kivuko cha MV Nyerere.

Akizungumza mjini hapa jana, Dk. Shoo, alisema: “Sisi kama kanisa tumeguswa sana na msiba huu wa kitaifa na tutaendelea kuwaombea wafiwa.

“Kwa masikitiko nawapa pole ndugu, jamaa, marafiki walioondokewa na ndugu zao, nampa pole Rais Dk. John Magufuli, kwa sababu huu ni msiba wa Taifa.

“Kwa niaba ya Kanisa la KKKT nawapa pole na wale manusura Mungu mwenyewe awaponye haraka.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here