27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Askofu Shao atoa neno malezi ya watoto

Na Masanja Mabula

-PEMBA

ASKOFU wa Kanisa Katoliki Zanzibar, Agustino Shao ameitaka jamii kuwalea watoto katika maadili mema na kuhakikisha wanawalinda na vikundi viovu ili kuwafanya wawe mashuhuda wa ukweli.

Amesema ni jukumu la kila mzazi na mlezi kuhakikisha mtoto wake anaishi kwa hofu ya Mungu kwa kufuata mafundisho ya dini.

Hayo aliyasema jana alipokuwa akizungumza na na watoto wa haki na amani katika maadhimisho ya kumbukumbu ya watoto mashahidi iliyofanyika kitaifa katika Kanisa Kuu la Wete Pemba.

Alisema wazazi wana jukumu la kumtayarisha mtoto kuweza kutambua leo yake paamoja na kesho yake, pamoja na kuwapatia elimu ambayo ndio mkombozi wao.

“Kila mzazi analojukumu la kuhakikisha mtoto wake anapata malezi bora ambayo yatamsaidia kuishi kwa hofu ya Mungu na kujiepusha na makundi maovu,” alisema

L;icha ya hali hiyo amelaani tabia ya baadhi ya wazazi ya kuwakosesha haki ya elimu watoto wa kike  na kusema wote wanahaki ya kupata elimu.

“Mipango ya Mungu ipo juu kulimo ya mwanadamu sasa ni lazima jamii ijenge imani ya kumtegemea Mungu katika kazi zao za kila siku,” alisema Askofu Shao.

Kwa upande wao walezi wa watoto wa haki na amani akiwemo, Frola Vicent na Jenister Mvula, walisema changamoto kubwa inayowakabili ni wazazi kutokuwa na mwamko wa kuwaruhusu watoto kushiriki utume.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles