Askofu Ruwa’ichi kuruhusiwa kutoka hospitali

0
650

Aveline Kitomary -Dar es salaam

ASKOFU Mkuu wa Jimbo Katoliki Dar es Salaam, Mhashamu Yuda Ruwa’ichi, anatarajiwa kuruhusiwa kutoka hospitali baada ya afya yake kuimarika.

Mmoja wa madaktari wanaomhudumia, Dk. Henry Humba aliiambia MTANZANI Dar es Salaam jana kuwa Askofu Ruwa’ichi anaweza kuruhusiwa siku mbili au tatu zijazo.

“Hali inaendelea vizuri, amezidi kuimarika, sasa yuko wodi za kawaida anatembea, anakula, anatambua watu na pia anaongea kama zamani,” alisema Dk. Humba.

Askofu Ruwa’ichi alifikishwa Taasisi ya Moi akitokea Hospitali ya Rufaa KCMC mkoani Kilimanjaro Septemba 9, mwaka huu saa 5 usiku  ambako alifanyiwa upasuaji mkubwa wa ubongo na madaktari bingwa watatu ndani ya sasa tatu.

Daktari mwingine kati ya waliomfanyia upasuaji, Profesa Joseph Kahamba alisema Askofu Ruwa’ichi alikuwa anasumbuliwa na tatizo la damu kuvuja kwenye ubongo linalojulikana kitaalamu ‘Chronic Subdural Hematoma’.

Alisema tatizo hilo linatokea baada ya mishipa ya damu kupasuka na damu kuvuja ndani ya ubongo, huku sababu zikiwa ni kuumia sehemu ya kichwa, shinikizo la juu la damu la kupanda na matumizi ya dawa za maumivu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here