Askofu Ruwa’ichi afanyiwa upasuaji mkubwa wa kichwa

0
1003

Mwandishi wetu – Dar es Salaam

TAASISI ya Mifupa Muhimbili (MOI), imesema Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Dar es Salaam, Askofu Yuda Ruwa’ichi, amefanyiwa upasuaji mkubwa wa kichwa usiku wa kuamkia jana.

Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na MOI, Askofu Ruwa’ichi alipokewa hospitalini hapo juzi saa tano usiku akitokea Hospitali ya KCMC Moshi mkoani Kilimanjaro.

“Baada ya kupokewa, wataalamu wa MOI  walimfanyia uchunguzi na vipimo kubaini alihitaji upasuaji wa dharura.

“Jopo la madaktari bingwa pamoja na wauguzi wa taasisi ya MOI walimfanyia upasuaji mkubwa kwa muda wa saa tatu kuanzia saa 7 usiku hadi saa 10 alfajiri, upasuaji huo ulifanyika kwa mafanikio makubwa,” ilisema taarifa hiyo.

Ilisema baada ya upasuaji, afya ya Askofu Ruwa’ichi inaendelea vizuri na kwamba bado yupo kwenye chumba cha uangalizi maalumu (ICU).

“Taasisi ya MOI inawatoa hofu Watanzania wote, hususani waumini wa Kanisa Katoliki kwamba hali ya Askofu Ruwa’ichi inaendelea vizuri na tumwombee ili aweze kupona mapema na kurejea kwenye majukumu yake ya utumishi,” ilisema taarifa hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here