31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Askofu Romero, Papa Paul VI watangazwa kuwa watakatifu

VATICAN CITY,Vatican

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani, Papa  Francis amewatangaza kuwa watakatifu, Askofu Mkuu aliyeuawa  El Salvado,  Óscar Romero na Papa John Paulo VI .

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Papa Fransis alimtangaza kiongozi huyo wa zamani jana  katika ibada.

Alimsifia kwa kuwa balozi wa amani  wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe  nchini humo na kujitoa sadaka kuwa karibu na maskini na watu wake.

Askofu  Romero aliuawa mwaka 1980 na wanajeshi wakati akiendesha ibada na hadi sasa  wauaji wake hawajawahi kufikishwa  kwenye vyombo vya sheria.

Mbali na Askofu mkuu huyo, Papa  Francis vilevile alimtangaza Papa  Paul VI, kwa mchango alioufanya katika kuleta mabadiliko  katika Kanisa Katoliki miaka  ya  1960.

Mwandishi wa BBC nchini humo, Will Grant alisema  hatua ya Askofu Romero  kutangazwa kuwa mtakatifu imekuwa ikiombwa na na Wakatoliki wengi  katika nchi hiyo.

“Sisi tunatangaza na kuwaelezea Papa Paulo VI na Óscar Arnulfo Romero Galdámez … kuwa watakatifu na tunawaandikisha kati ya watakatifu kwa sababu  wanapaswa kuheshimiwa  na kanisa lolote,” kiongozi mkuu huyo wa Katoliki aliuambia umati wa watu wapatao  60,000 walihohudhuria ibada hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Mtakatifu Petro.

Pia katika ibada hiyo kiongozi huyo aliwatangaza watu wengine watano kuwa wenye kheri akiwamo yatima aliyefariki duni  kwa saratani ya mifupa na mtawa mmoja raia wa Ujerumani.

Maelfu ya mahujaji walijitokeza kutoa heshima kwa watakatifu hao wapya wakiwamo  5,000  raia wa El Salvado.

BBC ilieleza kuwa Askofu Romero  alitangazwa kuwa mwenye kheri Mei 2015  katika ibada iliyofanyika El Salvador na  kuhudhuriwa na maelfu ya waumini wa kanisa hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles