24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Askofu Pengo arudishwa tena Muhimbili

pengoNa Veronica Romwald, Dar es Salaam

ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, amelazwa tena katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Uhusiano Msaidizi wa MNH, Neema Mwangomo, alisema Kardinali Pengo alifikishwa hospitalini hapo jana saa nne asubuhi.

“Askofu aliletwa jana saa nne asubuhi na alilazwa katika kitengo chetu cha dharura ambapo madaktari walikuwa wakimfanyia uchunguzi wa afya yake,” alisema.

Siku chache zilizopita, Askofu Pengo alilazwa katika Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyoko hospitalini hapo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.

Januari mosi, mwaka huu Rais Dk. John Magufuli pamoja na mkewe, Janeth walikwenda kumjulia hali askofu huyo.

Askofu Pengo aliruhusiwa kurudi nyumbani Januari 8 baada ya madaktari kuridhishwa na afya yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles