24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Askofu Nkwande awakemea viongozi

 CLARA MATIMO– MWANZA

ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, Renatus Nkwande, amekemea tabia ya baadhi ya viongozi waliopewa dhamana ya kuongoza katika sekta mbalimbali ambao wanatumia madaraka hayo kwa manufaa yao binafsi.

Pia ameitaka jamii kuendelea kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona kwa kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya, viongozi wa Serikali na dini bila kusahau kumuomba Mwenyezi Mungu ili janga hili liishe upesi.

Askofu Nkwande aliyasema hayo jana jijini hapa wakati akihubiri kwenye Misa Takatifu ya Jumapili katika Kanisa la Epifania Parokia ya Bugando Jimbo Kuu la Mwanza iliyolenga kuombea miito mbalimbali kwa viongozi.

Alisema viongozi wenye tabia ya kujinufaisha wenyewe wajitafakari wao ni wachungaji wa aina gani kwa sababu Yesu Kristo alikuwa ni mchungaji mwema.

“Bwana Yesu alipoanza kazi kitu cha kwanza alichokifanya alichagua mitume alikuwa anafanya mpango wa kuandaa watu wamrudie Mwenyezi Mungu, kinachotakiwa ni unyofu, unyenyekevu na utii.

“Lakini wapo baadhi ya watu wakipewa madaraka wanajilimbikizia mali, wengine wanaiba matirioni ya pesa wakati kuna wananchi wenzao hawana uwezo hata wa kununua daftari la shule la watoto wao, ndugu zangu mchungaji mwema ni yule ambaye anasimamia kweli, yuko tayari kulaumiwa na kutukanwa,” alisema.

Akihamasisha waumini kujikinga na ugonjwa wa corona, Askofu Nkwande, aliitaka jamii kutokuwa na hofu kwasababu majanga yote yanayotokea duniani ni mpango wa Mungu anataka wanadamu waache dhambi na wamrudie.

“Hofu ya kweli ni hofu ya Mungu nje ya hiyo ni dhambi.Tujue Mungu anampango na sisi kwa kuleta janga la corona, watakaokufa na watakaobaki wote ni wa Mungu maana Mungu hanyeshei mvua kwa watu wema tu hivyo unaposali usijiombee peke yako bali sali ili ulimwengu upone tusijifiche tukijificha shetani atatamalaki,” alisema.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles