31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Askofu Niwemugizi amjibu Migiro

Dk.-Asha-Rose-Migiro-Na Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam
ASKOFU wa Jimbo Katoliki la Rulenge mkoani Kagera, Seveline Niwemugizi amesema, viongozi wa dini wana haki ya kuwaelimisha waumini wao waweze kujua kinachoendelea wanapoona kuna mambo hayaendi sawa katika jamii.
Niwemugizi alisema pia wanayo haki ya kuwaambia waumini wao kuipigia kura ya Hapana, Katiba Inayopendekezwa kwa sababu ni wajibu wao kufanya hivyo.
Akizungumza na MTANZANIA kwa simu jana, askofu Niwemugizi, alisema wao kama viongozi wa jamii hawawezi kuona waumini wao wanapotea halafu wanakaa kimya.
Kufanya hivyo kutasababisha waingie kwenye uovu, alisema.
Askofu Niwemugizi ametoa kauli hiyo siku moja baada ya Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro kuwataka maaskofu wasiwafundishe wananchi jinsiya kupiga kura bali wawaache watumie haki yao ya katiba kupiga kura kulingana na utashi wao wenyewe.
“Sisi ni viongozi wa dini hatuwezi kuwaona kondoo wa Bwana wanapotea halafu tukakaa kimya au kuwaacha, tutakuwa hatujatenda haki, lazima tuwaambie waweze kuondoka kwenye kundi hilo na waweze kujitambua,”alisema askofu huyo ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC).
Alisema hata viongozi wa serikali wanawaambia wananchi waipigie kura ya NDUYO, Katiba Inayopendekezwa kwa sababu inalinda masilahi yao na kuhoji haki hiyo ya kuwaelekeza hivyo wananchi wameipata wapi?
“Nimeshangaa kusikia kuwa Waziri anasema viongozi wa dini hatuna haki ya kuwaambia waumini kuipigia kura ya hapana Katiba Inayopendekezwa, mbona Serikali imewaambia wananchi waipigie kura ya ndiyo, haki hiyo wameitoa wapi,” alihoji.
Juzi, Waziri Migiro aliunga mkono kauli ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, ambaye aliwataka viongozi wenzake wa dini kuacha kuwafundisha waumini kupiga kura ya hapana, bali waumini hao wanapaswa kufanya uamuzi wao kwa utashi wao wenyewe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles