27.7 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

ASKOFU MOKIWA AOMBA USULUHISHI NJE YA MAHAKAMA

 

Na Kulwa Mzee

-Dar es Salaam

ALIYEKUWA Askofu wa Anglikana Jimbo la Dar es Salaam, Valentino Mokiwa amewasilisha barua mahakamani akiomba kuondoa kesi aliyofungua akipinga kustaafishwa kwa nguvu ili wakamalizane katika nyumba ya maaskofu.

Mokiwa anataka kuondoa kesi hiyo ya madai namba 20, ya mwaka huu aliyofungua dhidi ya Askofu Mkuu wa Makanisa ya Anglikana Tanzania Mhashamu Dk. Jacobe Chimeledya na Bodi ya Wadhamini ya kanisa hilo.

Katika maombi yake ya leo, Askofu Mokiwa anaiomba mahakama kuiondoa kesi hiyo ni kutokana na juhudi za kutatua mgogoro huo katika nyumba ya maaskofu kwani usuluhishi hauwezi kufanyika bila kesi hiyo kuondolewa mahakamani.

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Thomas Simba amesema hajaiona barua hiyo na kwamba kesi hiyo ilipangwa Februari 28 hivyo kuwepo kwao jana mahakama haitambui.

“Leo mliitwa na nani, mimi siandiki kitu, niandike ili iweje, siwahitaji, kesi imepangwa tarehe 28, pisheni wengine waendelee, naona kuna barua ya kumalizana katika nyumba ya maaskofu, kama ni hivyo nawaombea usuluhishi mwema,”alisema Hakimu Simba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles