Brighiter Masaki -Dar es salaam
ASKOFU Mkuu wa kanisa la Adverntist Wasabato, Mark Malekana, amewataka viongozi wa dini kuhubiri maisha halisi ya watanzania nasio kuwahubiri utajiri peke yake.
Alisema hayo wakati akitambulisha gazeti la kanisa hilo linalojulikana kwa jina la Sauti Kuu, muumini kutojifunza neno peke yake bali wanatakiwa kujuwa na kufatilia habari za Afya, uchumi na Siasa.
Akizungumza na waandishi wa habari, mapema leo Malekana alisema kuwa kazi kubwa ya kanisa nikupeleka habari za kiroho, afya, tiba, elimu mbalimbali, siasa, uchumi na nyinginezo zenye maslahi katika jamii kiujumla.
”Maisha halisi ya mtanzania ni kuishi kwa kutafuta kipato cha kawaida unavyomuhubiria kuwa apokee gari wakati hata baskeli hana ni jambo la kumfanya aende tofauti na maisha yake halisi”.
”Muumini unae mfundisha mambo ya kiroho usiuwe, usizini,usiibe huku yeye analala njaa hawezi kukuelewa wakati unatakiwa kumwelekeza jinsi ya kubadili mtindo wake wa maisha, mwambie acha kuiba na mfundishe jinsi ya kutafuta pesa na afanyaje kazi ili aweze kukizi haja zake” anasema Malekana