30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

ASKOFU MANASE: KILA KANISA LIKITOA WARAKA WAKE TAIFA HALITAKALIKA

Na Eliya Mbonea, Arusha

Askofu Mkuu wa Makanisa ya Babtisti Tanzania, Mchungaji Arnold Manase amewataka viongozi wa dini kushauri kwa namna njema bila kutabiria nchi mambo mabaya kwani ubaya huenea haraka kuliko wema.

Aidha, amesema kila dhehebu nchini likisimama na kutoa waraka wake taifa halitakalika.

Askofu Manase ameyasema hayo leo Jumapili Aprili Mosi, jijini Arusha wakati akitoa salam kwenye Ibada ya Pasaka katika Kanisa la Jerusalem Babtisti lilipo Ngarenaro mjini Arusha.

Kupitia Ibada hiyo, Askofu Manase amewaomba wadau wa amani nchini, ikiwamo Serikali kukaa na wadau ili kujadili mustabali wa taifa.

“Tunahitaji kuomba amani ya Mungu itawale, kama ambavyo Yesu Kristo alivyotuachia amani yake.

“Tukiwa kama viongozi wa dini kama kuna mambo tunaweza kushauri basi tuyashauri kwa namna njema tusitabirie nchi mambo mabaya Kwani ubaya unaenea haraka kuliko wema, nawasihi tuhubiri amani,” amesema Askofu Manase.

Pamoja na mambo mengine, Askofu Manase katika Ibada hiyo ameongoza maombi kuomba hekima kwa viongozi wa Serikali, madhehebu yote nchono ili hekima ya Yesu Kristo ikatawale kwenye mioyo yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles