ASKOFU GWAJIMA APATA KIGUGUMIZI

0
568

Na Mwandishi wetu – Dar es Salaam

ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, amesita kuzungumzia kutajwa kwa jina lake katika orodha ya watu 65 wanaotuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya.

Alipotafutwa kwa simu na MTANZANIA jana kuzungumzia suala hilo, Askofu Gwajima alimtaka mwandishi ampigie baada ya muda ili apate wasaa wa kutafakari kauli ya kutoa.

“Kuhusu hilo suala, nipigie baadae kidogo, nadhani nitapata muda mzuri wa kuzungumza,” alisema Askofu Gwajima.

Hata hivyo, MTANZANIA ilipomtafuta kwa mara ya pili, hakupokea simu na alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno hakuujibu na mwishowe alizima simu.

Hata hivyo wakati tunakwenda mtamboni taarifa zilizotufikia Askofu Gwajima atazungumza leo na vyombo vya habari.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here