26.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, January 18, 2022

ASKOFU GWAJIMA AFUTIWA KESI YA KUMTUKANA KARDINALI PENGO

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia huru Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima katika kesi ya kutoa lugha ya matusi dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Gwajima ameachiwa huru leo baada ya mahakama kuifuta kesi hiyo kwa sababu upande wa Jamhuri umeshindwa kuonesha kujali kwani kwa miezi 14 wameleta shahidi mmoja kutoa ushahidi.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Cyprian Mkeha, ametoa uamuzi huo leo wakati kesi hiyo ilipokuja kwa kusikilizwa huku upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Joseph Maugo, ukiomba upewe ahirisho lingine kwa kuwa hawakuwa na shahidi.

Mkeha aliamua kuifuta kesi hiyo kwa kutumia kifungu cha 225 cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (CPA) na kumwachia huru Gwajima.

Alisema upande wa Jamhuri umeshindwa kuonesha kujali shauri hilo ambapo ndani ya miezi 14 umeita shahidi mmoja tu.

Gwajima alipandishwa kizimbani mahakamani  Aprili 17,2015 akidaiwa kati ya Machi 16 na 25, 2015, katika viwanja vya Tanganyika Packers, vilivyopo Kawe jijini Dar es Salaam, alitoa lugha ya matusi kwa Kardinali Pengo.

Alitamka:  "Mimi Askofu Gwajima nasema Askofu Pengo ni mpuuzi mmoja yule, mjinga mmoja, amekula nini yule, sijui amekula nini yule mtoto hana akili yule..”

Previous articleNI MTIKISIKO BUNGENI
Next articleJPM: MTANIKUMBUKA

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
174,922FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles