28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

ASKOFU ATAKA RAIS ASAIDIWE

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la The Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT), Dk. Brown Mwakipesile amewataka viongozi wa madhehebu ya dini kumsaidia kwa nguvu zote Rais Dk. John Magufuli  kupambana na maovu.

Askofu Dk.Mwakipesile, alitoa kauli hiyo juzi wakati alipokuwa akifungua kongamano la kitaifa la siku nne la The Evangelist Assemblies of God Bodi of Evangelistic (TEBE), lillilofanyika katika kanisa EAGT Mlimwa West Mkoani  Dodoma.

Kongamano hilo ambalo limewakutanisha zaidi ya watumishi 700, wakiwamo maaskofu,wachungaji,wainjilisti na wakuu wa idara.

Alisema vitendo vinavyojitokeza ndani ya nchi hii, kama vile masuala la vyeti vya kungushi ,madawa ya kulevya, viroba, watumishi hewa na mengineyo, bila kumsaidia kamwe haviwezi kukoma.

 ‘’Rais anahitaji msaada wa viongozi wa dini na nyie mpo kimya, lazima tumsaidie katika maombi pamoja na kupaza sauti katika vyeti feki, dawa za kulevya bila kumsaidia kamwe haviwezi kukoma,’’alisema

Alisema viongozi wa dini wakishirikiana kwa pamoja na serikali iliyopo madarakani kusimamia kwa uaminifu kwenye maeneo yao, wataisababishia serikali kuifanya kazi yake kwa uhuru na watu wake watafanya kazi kwa bidii.

“Vitendo vinavyojitokeza na kuchafua sura ya Taifa letu, ni kwa sababu viongozi wa dini wamekaa kimya,basi mnatakiwa kusimama kwa uaminifu katika maeneo yenu ya utumishi ili kuweza kumsaidia rais wetu katika kupambana na haya maovu”alisema.

Alisema kama watajisimamia na kuhubiri injili ya ukweli na uwazi watakuwa wametoa mchango mkubwa katika kupambana na uovu unaofanywa na watu wachache.

“Tukitimiza wajibu wetu,Serikali na Rais haiwezi kupata shida  ya kuwabaini wanaotenda hayo maovu yanayojitokeza ndani ya nchi yetu,’’alisema.

 

MWISHO

 

DC akerwa wananchi kujaza mawe kwenye visima

 

NA FLORENCE SANAWA, NANYAMBA

 

MKUU wa Wilaya ya Mtwara, Avod Mmanda amesikitishwa na kitendo na wananchi wa vijiji vya Kilomba na Mikumbi Halmashauri ya Mji ya Nanyamba kuweka mawe ndani ya visima hatua ambayo  itaigharimu halmashauri hiyo kutengeneza upya.

Akizungumza wakati wa kikao cha kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya Mji wa Nanyamba juzi, baada ya kupata taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Oscar Ng’itu.

Alisema hatua hiyo haikubaliki wala haidhirishi.

Alisema  hatua hiyo ya wana kijiji kuweka mawe imesababisha halmashauri hiyo kushindwa kusafisha visima, badala yake wametakiwa kutumia mamilioni ya fedha kuchimba visima  vipya.

 “Nitakwenda Kilomba na Mikumbi mwenyewe nikajiridhishe, hii hadithi ya kujaza mawe kwenye visima sijaielewa na sijaridhishwa nataka nikashuhudie mwenyewe je, kuna mawe yamejazwa kwenye visima au ni maneno.

“Hili ni jambo lenye kusikitisha Tanzania ya leo kisima cha maji kinawekewa mawe,maji ni uhai kama kuna watu wamefanya  wachukuliwe, lazima mwenyekiti wa kijiji atupe maelezo ilikuwaje kisima kijazwe mawe hadi kishindwe kusafishwa? alihoji Mmanda.

 

Naye Diwani wa Kata ya Nanyamba, Hassan maauji alisema tatizo la maji limeongezeka  kubwa pamoja na Serikali kuwasogezea umeme kwenye chanzo cha maji ambacho walikuwa wakitumia genereta awali.

Alisema mabadiliko ya matumizi ya nishati ya kuendesha miradi wa maji bado hali imekuwa tete kwa kuwa wamekuwa hawaoni ya mabadiliko hayo.

“Hapa inabidi tushirikiane kila mmoja afanye sehemu yake bila kuwapo kwa usumbufu ili  kuwatumikia wananchi, hatuwezi kukaa kimya, wakati wananchi  hawana huduma ya maji kwa sababu ambazo zinaweza kuzuilika,” alisema Mauji

Kwaupande wake Mkurugenzi wa Halmashuri hiyo, Oscar Ng’itu alisema  hadi sasa wamekwama kufanya usafi katika visima vitatu kati ya 17 vilivyotakiwa kufanyiwa matengezo.

“Hatuwezi kuzikataa changamoto za maji kuwa hazipo kwetu zipo tu ila tuna miradi mikubwa ambayo itasaidia vijiji vyote ambapo tunaendelea kuboresha na vyanzo vyetu vya maji vya ndani ingawa kuna visima vitatu ambayo vimeonekana na kuwa na mawe hivyo kushindikana kufanyiwa usafi,” alisema Ng’itu

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles