28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 21, 2024

Contact us: [email protected]

Askari wadaiwa kujeruhi na kuua waandamanaji 20 Nigeria

Lagos, Nigeria 

WATU kadhaa walioandamana dhidi ya polisi, wameripotiwa kupigwa risasi na kufa na huku wengine wakiwa wamejeruhiwamjini Lagos nchini Nigeria.

Walioshuhudia tukio hilo wameiambia BBC kuwa wameona miili 20 ilikuwa imetapakaa na wengine 50 wamejeruhiwa baada ya wanajeshi kufyatua risasi.

Shirika la kimataifa la Amnesty limesema limepata habari za kuaminika kuhusiana na vifo hivyo.

Maofisa wameahidi kufanya uchunguzi kuhusu shambulio hilo.

Amri ya kutotoka nje ndani ya saa 24 imewekwa mjini Lagos na miji mingine.

Waandamanaji sasa wamezunguka vituo vya polisi, kikosi maalum cha Sars, kimekuwa kikiendelea kwa muda wa wiki mbili .

Kutokana na mapigano ya risasi yanayoendelea , aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Marekani Hillary Clinton amemtaka Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kuacha kuwaua vijana asitishe maandamano ya Sars.

Mcheza mpira Nigeria Odion Jude Ighalo, ambaye anaichezea Manchester United, ameishutumu serikali ya Nigeria kwa kuua wananchi wake.

Alisema hayo kupitia ukurasa wa tweeter kwa kuweka video.

Walioshuhudia tukio hilo walizungumzia wanaume ambao hawakuwa katika sare ambao walipiga risasi jioni ya siku ya Jumanne.

Askari wenye silaha walikuwa wakiwazuia waandamanaji kabla ya risasi kuanza kupigwa , mwandishi wa BBC Nigeria Nayeni Jones anaripoti.

Video katika mitandao ya kijamii ilikuwa ikionesha tukio hilo mubashara.

Shuhuda ambaye hakutaka jina lake kutajwa aliiambia BBC kuwa majira ya saa moja kasoro usiku walianza kupiga risasi katika maandamano ambayo yalikuwa ya Amani.

Walikuwa wanapiga risasi moja kwa moja kwetu, lilikuwa tukio baya . Kuna mtu alipigwa risasi na kufa hapo hapo.

Walipiga risasi kwa muda was aa moja na nusu na baada ya hapo askari walichukua miili ya waliouawa.

Askari walikuwa wameweka zuio kwa waandamanaji hivyo magari ya wagonjwa yalishindwa kufika katika eneo la maandamano.

Askari walikuwa wameweka zuio kwa waandamanaji hivyo magari ya wagonjwa yalishindwa kufika katika eneo la maandamano.

Watu wengine wanne walioshuhudia waliiambia Reuters news agency kuwa askari waliwapiga risasi waandamanaji .

Mmoja wao Alfred Ononugbo, 55, alisema: “Walianza kupiga risasi katika mkusanyiko huo .

Niliona risasi zikipiga watu wawili.

Katika ujumbe wa tweet wa , Amnesty International Nigeria wamesema kuwa wana ushahidi tosha unaoonesha polisi wakitumia mabavu dhidi ya waandamanaji mjini Lagos”.

Msemaji wa Amnesty International Isa Sanusi alisema wana video inayoonesha polisi wakiwaua wananchi, wanajaribu kuhakiki ni wangapi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles