28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

ASKARI PORI LA AKIBA KIZIMBANI KWA RUSHWA

Na MOHAMED HAMAD, KITETO


ASKARI wanne wa Pori la Akiba la Mkungunero, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Kiteto kwa tuhuma ya kushawishi na kuomba rushwa ya Sh milioni tano kutoka kwa wafugaji ambao mifugo yao ilikamatwa ndani ya pori hilo.

Akisoma hati ya mashtaka ya watuhumiwa hao, Mwendesha mashataka wa Takukuru Mkoa wa Manyara, Isdory Kyando mbele ya Hakimu Mkazi, Hudi Majid, alidai   tukio hilo lilitokea Mei 12 mwaka huu katika Kijiji cha Ilkiushbouir wilayani Kiteto.

Kyando aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Martenus Mahoka, Augustino Sadick, Ephrahim Polepole na Godfrey Matheas wote askari wa Pori la Akiba la Mkungunero.

Alidai fedha hizo waliziomba kutoka kwa wenye mifugo waliokuwa wamekamatwa ndani ya Pori la Akiba la Mkungunero waweze kuiachia mifugo199  wakiwamo ng’ombe, mbuzi, kondoo na punda.

Kyando alidai washtakiwa hao kwa pamoja wanatuhumiwa kutenda kosa kwa mujibu wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007 kifungu cha 15 (1),

Washtakiwa hao   kwa pamoja walikana mashitaka  na walipata dhamana   hadi Septemba 17 mwaka huu kesi yao itakapotajwa tena.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles