26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Askari polisi mbaroni kwa tuhuma za wizi mauaji

Na ELIUD NGONDO -MBEYA

JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wanne akiwemo askari polisi mmoja kwa tuhuma za kumuua mwendesha pikipiki pamoja na kujihusisha na matukio ya wizi.

Akizungumza jana mjini hapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei alisema tukio hilo limetokea Juni 20, mwaka huu saa tatu usiku katika nyumba ya kulala wageni ya “The Governor City Lodge” iliyopo Iwambi jijini hapa.

Kamanda Matei aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni askari polisi mwenye namba G.8695 PC John Kaijage (34) mkazi wa Isyesye, Fotunatus Kagande (23), Petson Daniel (22) mkazi wa Iwambi na Jastini Kagande (27) mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. John  ambao wote ni wakazi wa Iwambi.

Alisema watuhumiwa hao wanatuhumiwa kwa kumuua Erasto Mwalwego (29) ambaye ni dereva pikipiki ambaye alikuwa mkazi wa Nzovwe jijini Mbeya.

Kamanda Matei alisema jeshi hilo lilipofanya uchunguzi wa awali limeweza kubaini kuwa mwili wa Mwalwego ulikuwa umejeruhiwa sehemu mbalimbali kwa kitu butu.

Alisema kabla ya kufikwa na mauti, Mwalwego alipelekwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa matibabu na Juni 21, mwaka huu saa 12 asubuhi alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu.

Kamanda Matei alisema upelelezi wa shauri hilo unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.

Aidha katika tukio jingine Kamanda Matei, alisema kuwa Juni 21, mwaka huu huko katika Kijiji cha Kilwa kilichopo Kata ya Kajunjumele, Wilaya ya Kyela, polisi walimkamata Bahati Ndinagwe (21) akiwa na barua ya kughushi.

Kamanda Matei alisema baada ya jeshi hilo kuikagua lilibaini kuwa inaonyesha kuwa imetoka katika Ofisi ya Usalama wa Taifa Makao Makuu kwenda kwa mtuhumiwa huyo ikimjulisha kuwa ameteuliwa kujiunga na idara hiyo.

Alisema lengo la barua hiyo ni kutaka kupata ajira hiyo kwa mbinu ovu ambapo mtuhumiwa alichapa barua hiyo kwa namna inayofanana na barua za idara hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles