22.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Askari polisi adaiwa kumbaka mwanafunzi na kumpa mimba

Na Ibrahim Yassin

-Mbeya

ASKARI polisi Daniel Mlanda, amedaiwa kumbaka mwanafunzi wa kidato cha kwanza mwenye miaka 14, na kutoroka katika kituo chake cha kazi, Kyela mkoani hapa.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Sebastian Mbuta, alithibitisha kuwapo kwa tuhuma hizo na kwamba kwa sasa wanazifanyia kazi.

Mwanafunzi huyo alidai kuwa alikuwa akibakwa na askari huyo akiwa katika lindo kwa shinikizo la mama yake mlezi ambaye walikuwa na urafiki.

Naye Said Mohammed ambaye ni mjomba wa mwanafunzi, alisema alipoona mpwa wake ameanza uvivu wa kwenda shule, alianza kumfuatilia na akagundua kwamba ana uhusiano na askari huyo.

Alisema alipomuhoji alikiri kuwa na mahusiano ya kimapenzi na askari huyo na kwamba ana ujauzito wake. 

Aisha Mohammed ambaye ni mama mzazi wa mwanafunzi huyo, alisema walivyopata taarifa za ujauzito wa mwanaye, walimuhoji na akasema alipewa na askari huyo baada ya kumwingilia bila ridhaa yake.

“Alisema mara ya kwanza aliingiliwa kinguvu na askari huyo na baadaye alimgeuza kama mkewe na ndiyo akampa na ujauzito,” alidai.

Hata hivyo, baada ya taarifa hizo kuvuja, imeelezwa kuwa vikao vya siri vilianza kufanyika ili kuficha tukio hilo licha ya wananchi kutaka hatua za kisheria zichukuliwe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles