24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Askari Magereza anaswa kwa utapeli CCM, asimamishwa kazi

NA BENJAMIN MASESE – MWANZA

ASKARI wa jeshi la magereza, Kibemba Warioba (27) mwenye namba B.9205 WDR amekamatwa na jeshi la polisi mkoa wa Mwanza  kwa kosa la kuanzisha Chama cha Ushirika cha Akiba cha na Mikopo (Saccos) cha info tell CCM na kuwatapeli wanachama wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza, leo Mei 26, Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Jumanne Murilo amesema askari huyo alikamatwa jana baada ya kupokea taarifa kwa wanachama wa CCM kwamba kuna saccos ya info Tell CCM inayotoa gawio kwa wanachama wa chama hicho.

“Askari huyo alikuwa anafanya kazi katika gereza la Biharamulo mkoani Kagera, kabila lake ni mzanaki, mpaka sasa tunavyozungumza  na nyinyi tayari tumewasiliana na viongozi wa jeshi la magereza na amesimamishwa kazi ili kuendelea na uchunguzi na kumfikisha mahakamani.

“Shughuli hii si kwamba alikuwa anaifanya yeye mwenyewe bali na watu wengine na baadhi yao tumewakamata ambao wamewatapeli wanachama wa CCM wakiwaeleza kuwa watapata gawio zuri na maisha yao yatakuwa mazuri na bora.

“Mtumishi huyu ameichafua sura ya jeshi la magereza, serikali na jina la chama cha  CCM, hatuwezi kuvumilia watu wa aina hii kuendelelea kufanya uhalifu na utepeli, tutawashughulikia na kama kuna watu wenye nia ya kujihusisha na shughuli isiyo halali ni vema wakaiacha,”amesema Kamanda Murilo.

Kamanda Murilo amesema baada ya taarifa hiyo kupokelewa, askari wa Mwanza walishirikiana na askari wa Mkoa wa Kagera walifuatilia mwanzilishi wa Saccos hiyo na kufanikiwa kummkamata askari huyo wa magereza akiwa na  laini za simu tano zikiwa zimesajiliwa kwa majina tofauti tofuati.

Amesema baada ya uchunguzi dhidi ya askari huyo wa magereza alikiri ndiye mhusika na tayari amewatapeli wanachama wa CCM wengi na watu wengine wa kawaida  huku akitambulisha kwa vyeo mbalimbali  vilivyopo ndani ya CCM na serikali.

Hata hivyo Kamanda Murilo aliwataka wanachama wa CCM na watu wengine ambao wametapeliwa na saccos hiyo kufika katika vituo vya polisi vya polisi kutoa taarifa zao ili waweze kurejeshewa fedha zao na hata kutoa ushahidi pale mtuhumiwa atakapofikishwa mahakamani.

Wakati huo huo watu 29 wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa makosa mbalimbali yakiwamo mauaji ya wavuvi, wizi, unyang’anyi na upatikanaji wa dawa za kulevya aina ya bangi na mirungi.

Kamanda Murilo amesema miongoni mwa watuhumiwa hao, wapo watu wawili ambao ni wavuvi wamekamatwa kwa tuhuma za mauaji  katika kisiwa cha Ukara baada ya kuwavamia wavuvi  wenzao wawili ambapo waliwafunga kamba miguuni na mikononi na kuwatumbukiza ziwani.

“Mvuvi mmoja kati ya wale waliofungwa kamba amepoteza  maisha, wavamizi wamewapora  injini ya boti, kokoro moja ya kuvulia dagaa, tanki la mafuta, simu na vitu mbalimbali vyote vikiwa na thamani zaidi ya shilingi milioni tano.

Kamanda Murilo amewataja watuhumiwa wa tukio hilo ni Rernard Tungaraza, Andrew Masumbuki na wenzake Sabato Msita, Laurent Julius, Sherida Paul, Joseph Charles na Juma Lisenge ambao walikamatwa katika Kisiwa cha Goziba wakiwa wanatoroka na vitu  vya wizi.

Aidha ameongeza kuwa katika operesheni ya kiukamata waalifu iliyofanywa jana ya mkoani Mwanza, polisi walifanikiwa  kuwakamata watu watano kwa kosa la kupatikana na vifaa vya kutengeneza noti za fedha bandia  za Tanzania na dola ya Marekani.

Watuhumiwa hao ni  Elasui Masawe, Yohana Pastory, Mussa Abbas, George Vanace, Vanace Jeremia na  Athman Idd ambapo amesema baada ya uchunguzi watafikishwa mahakamani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles