ASKARI JWTZ, WENZAKE KIZIMBANI MAUAJI YA KONDAKTA WA DALADALA

0
736

NA AMINA OMARI, TANGA

ASKARI wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), MT 69500 Sajini Taji John Komba na wenzake watatu, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tanga kwa tuhuma za mauaji ya kondakta wa daladala.

Sajini Komba na wenzake, wanatuhumiwa kumuua kondakta wa daladala inayofanya safari zake kati ya Nguvumali na Raskazoni.

Wakisomewa shtaka la mauaji linalowakabili mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Hilda Lyatuu, Wakili wa Serikali, Donata Kazungu alisema Januari 26, mwaka huu katika kambi ya jeshi iliyoko eneo la Nguvumali, mshtakiwa Komba akiwa na wenzake wanadaiwa kumuua Salum Kassim.

akili Kazungu, aliwataja washtakiwa wengine kuwa ni Yohana Warioba, Bernard Nicholaus ambao ni askari mgambo katika kambi hiyo Adamu Juma na Sofia John ambao ni wanafunzi.

Hata hivyo, watuhumiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

Mwendesha mashtaka huyo, alidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na inatarajiwa kutajwa tena Februari 26, mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here