27.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Askari JWTZ auawa akitoka doria

Allan Vicent – Tabora

ASKARI wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Kikosi cha 262 Milambo mkoani Tabora, ameuawa na watu wasiojulikana muda mfupi baada ya kumaliza doria akiwa njiani kurudi nyumbani kwake.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, Laurian Albert, alimtaja askari aliyeuawa kuwa ni MT.117342 PT Samwel Machugu (28).

Kamanda Albert alisema kuwa tukio hilo limetokea jana saa 12 asubuhi huko maeneo ya Kidatu B, Kata ya Ipuli Manispaa ya Tabora.

Alisema mwili wa marehemu uliokotwa umbali wa kilometa moja kutoka nyumbani kwake ukiwa na majeraha matatu  kichwani yaliyosababishwa na kupigwa kitu chenye ncha kali.

Alieleza kuwa inadaiwa muda mfupi kabla ya kifo chake alikuwa kwenye doria shirikishi na wananchi wa mtaani kwake na baada ya kumaliza aliachana nao na kuelekea nyumbani kwake.

Alibainisha kuwa akiwa njiani alikutana na watu wanaodhaniwa kuwa vibaka ambao walimshambulia hadi kusababisha kifo chake na kisha kumpora simu ya mkononi.

Kamanda Albert alisema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na msako mkali kuwasaka waliohusika na tukio hilo.

Alitoa wito kwa wananchi wa mkoa kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za wahalifu ili hatua ziweze kuchukuliwa ikiwemo kupambana nao.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,608FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles