22.7 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Asilimia 74 wajifungulia vituo vya afya

Ramadhan Hassan-Dodoma

JUMLA ya wajawazito 813,923 sawa na asilimia 74 wamejifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa wizara kwa kipindi cha Julai hadi Desemba mwaka jana kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.

“Katika kipindi hiki, matarajio yalikuwa ni wajawazito 1,100,000 wangejifungua, hata hivyo takwimu zinaonyesha kuwa jumla ya wajawazito 813,923 sawa na asilimia 74 walijifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma,” alisema Ummy.

Kwa upande wa mahudhurio ya kliniki, alisema kuwa jumla ya wajawazito 797,803 sawa na asilimia 73 ya walengwa walifanya mahudhurio ya kliniki manne na zaidi kama mwongozo ulivyoelekeza.

Aidha, alisema kuwa asilimia 87.4 ya wajawazito sawa na kina mama 886,810 walipatiwa dawa za kukinga malaria na jumla ya 2,844,174 sawa na asilimia 84.6 walipewa dawa ya kuzuia upungufu wa damu (FEFOL).

Hata hivyo Ummy alisema kuwa wizara kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, ilihakikisha dawa muhimu za kuzuia na kutibu kifafa cha mimba na kukinga na kutibu kupoteza damu baada ya kujifungua, kutibu magonjwa kwa watoto chini ya miaka mitano uliimarika kwa zaidi ya asilimia 85.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,580FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles