30 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

Asilimia 70 mifumo unawaji imefanikiwa

Tunu Nassor Na Christina Gauluhanga , Dar es salaam

KAIMU Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Abdallah Mtinika amesema hadi sasa asilimia 70 ya mifumo ya unawaji mikono kisasa katika jiji hilo  awamu ya kwanza imekamilika ambapo mradi huo utagharimu Sh.milioni 129.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Mtinika alisema mifumo hiyo inatengeneza na wataalam wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM).

Mradi huo, utatekelezwa kwenye maeneo yenye mikusanyiko zaidi ya watu.

Alisema utengenezaji mfumo huo, ni msaada kutoka Shirika la Water Aid Tanzania ambapo ofisi yake  uliomba ili kuunga mkono jitihada za Rais Dk.John Magufuli kupambana na ugonjwa wa corona.

“Mifumo hii ya kisasa itafungwa sehemu za vituo na zenye mikusanyiko ya kisasa,Water Aid Tanzania watalipia miundombinu ya maji taka na Safi yanayoingia na kutoka,”alisema Mtanika.

Alisema awamu ya kwanza ya mradi,itatumia Sh milioni 129, kazi ya uchimbaji mitaro ya kupitisha maji na usimikwaji inaendelea.

Alisema mifumo sasa tayari imeanza kutumikia katika stendi ya mabasi yaendayo mikoani Ubungo (UBT), na wanaendelea na uchimbaji katika vituo vya mabasi yaendayo kasi Gerezani – Kamata, Kimara na Kivukoni.

Alisema kwa kutambua mahitaji halisi ya upatikanaji wa maji tiririka ambayo ni safi na salama katika kipindi hiki cha kupambana na ugonjwa huo,  ameomba aongezewe mradi huo na tayari amekubaliwa.

Alisema awamu ya pili ya mradi, utakaoanza muda si mrefu utafanyika katika kituo cha mabasi yaendayo Kusini cha Mbagala,  Kigamboni Kivukoni na  upande wa pili wa Posta, kituo cha mabasi, Simu 200 , Makumbusho na Soko la Kariakoo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,352FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles