23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Asilimia 70.6 ya Watoto hawana vyeti vya kuzaliwa Mwanza

Na Sheila Katikula, Mwanza

Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini nchini (RITA) wamesema kuwa mpaka sasa ni asilimia 29.4 pekee ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano mkoani Mwanza ndio wamesajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa huku asilimia 70.6 wakisalia hawana vyeti hivyo

Hayo yameelezwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Emmy Hudson wakati akizungumzia zoezi hilo wilayani Misungwi mkoani hapa na kusema kuwa takwimu hizo zinamaanisha usajili kwenye vituo unafanyika kwa kiwango kidogo na taarifa za wanaofanyiwa zoezi hili haziingii kwenye simu.

Alitaja sababu zingine zilizopelekea kiwango cha usajili kushuka mkoani hapa ni kuondoka kwa wasajili wasaidizi, kuhama vituo, kubadilishiwa majukumu na kutokuwepo na mfumo mahususi wa kukabidhi majukumu kwa anayekabidhiwa ofisi.

Emmy alisema  tangu kuanza kwa mpango huo mwaka 2013 mpaka sasa wametekeleza kwenye mikoa 20 ya Tanzania bara wamesajili na kutoa vyeti kwa watoto milioni 5.9 kwa mikoa miwili, Mbeya na Mwanza mpaka mwaka jana kuongeza kiwango cha Watoto cha walisajiliwa kutoka asilimia 13 mwaka 2012 hadi kufikia asilimia 55 mwaka 2020.

“Utekelezaji wa mpango  huu wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano katika Mkoa wa Mwanza ulianza mwaka 2015 kwani ulikuwa  mkoa wa pili kuanza zoezi hili, usajili ulifanyika kwenye vituo vya tiba tu tofauti na mikao mingine huduma zinapatikana kwenye ofisi za Watendaji wa Kata,” alisema.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa RITA, Patricia Mpuya alisema utekelezaji wa mpango huo unatekeleza zoezi la kutoa cheti  cha mtoto toleo la kwanza ambacho hujazwa kwa mkono na ni halali kwani mtoto anaposajiliwa hupewa namba maalum ya utambulisho ambayo hupatikana kwenye vyeti vilivyochapwa kwa mashine,” alisema Patricia.

Aidha Mwenyekiti wa  Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Mpandalume Simon alisema ili zoezi hilo liwe na ufanisi ni vyema likashirikisha wanasiasa, Watendaji wa vijiji, vitongoji, wasanii na viongozi wa dini kwa sababu  wanauwezo wa kukutana na wananchi mara kwa mara.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Luhumbi alizitaka halmashauri zote mkoani hapa kutumia mbinu mbadala na shirikishi zaidi kuhakikisha wanafanikisha zoezi hilo kuwezesha kuongeza kasi ya usajili wa watoto walio chini ya miaka mitano waweze kupata vyeti vya kuzaliwa ambapo aliipongeza halmashauri ya wilaya ya Misungwi kwa kupiga hatua kubwa katika hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles