23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

‘Asilimia 60 wananchi hawataki maandamano’

chadema

Na MWANDISI WETU, DAR ES SALAAM

TAASISI isiyokuwa na kiserikali ya Twaweza imesema asilimia 60 ya wananchi wanaunga mkono kuzuiwa kwa mikutano ya vyama vya siasa.

Ripoti hiyo iliyotolewa jana Jijini Dar es Salaam ilihusu maoni ya wananchi kuhusu demokrasia, udikteta na maandamano.

Ripoti hiyo iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam jana ilisema matokeo yake yametokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,602 kati ya Agosti 23 na 29 mwaka huu.

Kwa mujibu wa utafiti huo, asilimia 95 ya wananchi wana uthamini uwezo wa kuikosoa serikali huku wananchi saba kati ya 10 wakisema demokrasia ndio mfumo bora wa utawala.

Utafiti huo pia unaonyesha kuwa asilimia 60 ya wananchi wanakubali kuzuiwa kwa mikutano ya vyama vya siasa ikihusisha asilimia 70 ya wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na asilimia 33 ya wafuasi wa vyama vya upinzani.

Kuhusu ushiriki kwenye maandamano, asilimia 50 wamesema hawako tayari kushiriki huku asilimia 29 wakiwa tayari kushiriki.

Pia asilimia 80 ya wananchi wanasema baada ya uchaguzi vyama vya upinzani vikubali kushindwa na visaidiane na serikali kuijenga nchi.

Mbali na hilo asilimia 49 wanasema mikutano baada ya kipindi cha kampeni hukwamisha maendeleo huku asilimia 47 wakisema vyama vya upinzani viruhusiwe kufanya mikutano yao bila kipingamizi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze akizungumzia utafiti huo alisema, “Watanzania wengi wanauunga mkono mfumo wa demokrasia ya vyama vingi na uhuru wa kukusanyika na kutoa maoni. Kwa sasa, idadi kubwa ya wananchi hawakubaliani na kauli inayosema kuwa Rais Magufuli ni dikteta.”

Akizungumzia utafiti huo, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeuponda utafiti huo kikisema kuwa taasisi hiyo inaidanganya dunia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles