24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, March 29, 2023

Contact us: [email protected]

Asilimia 39 tu hunyonyesha maziwa ya mama pekee Misenyi

NYEMO MALECELA-BUKOBA

ASILIMIA 39 ya wanawake pekee wenye watoto chini ya miaka mitano wilayani Misenyi mkoani Kagera, ndio wanaonyonyesha watoto chini ya miezi sita maziwa ya mama pekee.

Hali hiyo imetajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa watoto chini ya miaka mitano kukabiliwa na udumavu.

Ofisa Lishe wa Wilaya ya Misenyi, Zainath Hassan, alisema hayo jana katika mkutano wa tathmini ya lishe ya Mkoa wa Kagera.

 “Harakati za kuondoa udumavu wilayani Misenyi zinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo upungufu wa bajeti ambapo mwaka 2018/19 wilayani Misenyi tulitenga bajeti ya Sh milioni 52, lakini halmashauri ilitupatia milioni 2 pekee.

 “Kutokana na kupewa kiasi hicho kidogo cha fedha, tumefanikiwa kutekeleza shughuli moja tu ya kijamii ya kuondoa udumavu wilayani hapa badala ya shughuli saba zilizokuwa zimepangwa kutekelezwa,” alisema.

Zainath alizitaja kata zilizoathirika zaidi na udumavu wilayani humo kuwa ni Kilimilile katika Kijiji cha Kenyana, Nyankere na Kasambya, Kijiji cha Itara, Mabuye na Gaburanga.

 “Katika Wilaya ya Misenyi, tunayo hospitali moja tu ya Mugana ndiyo inayotoa tiba kwa watoto wenye udumavu, hivyo ili kukabiliana na hali hiyo kwa watoto ambao hawawezi kufika katika hospitali hiyo, tumekuwa tukilitegemea Shirika la Ima World Health kupitia Mradi wa Mwerevu linalofadhiliwa na Serikali ya Uingereza kutoa elimu ya lishe ya jinsi ya kuandaa chakula dawa kwa watoto walioathirika,” alisema Zainath.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,259FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles