33.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ashinda Tuzo ya Nobel kwa kuishi kama mbuzi milimani

160923110044-02-goat-man-exlarge-169

Marekani.

Katika hali ya kustaajabisha lakini yenye kuwavutia wengi kijana,  Thomas Thwaites aibuka mshindi wa tuzo ya Ig Nobel baada yakuonyesha umahiri wa kuishi kama mbuzi kwenye Milima ya Alps kwa siku tatu.

Thomas aliishi kama mbuzi aishivyo akiwa amevalia kama wao kuwakilisha mradi wake uitwao ‘A holiday from being human (GoatMan).’

Kwa mujibu wa tovuti ya Ig Nobel, tuzo hizo zilizofanyika katika Chuo Kikuu cha Havard, Marekani juzi, zinalenga kuwafanya watu wafurahi, kufikiri na kushawishi umma kuamini katika sayansi.

Tuzo hizo za kejeli ambazo sio maarufu kama tuzo za kweli za Nobel hufanyika kila mwaka na zimehamasishwa na jarida la burudani la kisayansi nchini Marekani kupitia tafiti zake.

Hata hivyo tuzo hizo zilitolewa kwa washiriki wengi wakiwemo  watafiti waliowavalisha panya suruali za pamba ili kufahamu maisha yao ya uhusiano pia wanasayansi waliotafiti tabia za miamba.

“Ni moja ya tukio la ajabu ambalo linakuwa limefanana sana na tuzo maarufu duniani za Nobel lakini huku wanasayansi wa kweli wanapewa tuzo kwa kufanya mambo ya ajabu, inavutia,” alisema Amanda Palmer, mmoja wa watumbuizaji na mwandishi.

Katika kuipa taswira ya kusisimua tuzo hii, watazamaji huwa wanarusha ndege za makaratasi kwenye jukwaa wakati baadhi ya washindi wa tuzo hizo wakiwa jukwaani na mavazi rasmi yaliyowakilisha tafiti zao.160923094040-01-ig-nobel-2016-exlarge-169

Mbali na tuzo 10 zinazotolewa kila mwaka, mambo mengine yaliyoongezwa kwenye tuzo za mwaka huu ni pamoja na tuzo kwa timu ya Ujerumani waliogundua namna yakutibu maumivu ya mwili kupitia kioo.

Vilevile, tuzo ya mtazamo ilienda kwa watafiti wa kijapani waliotafiti kama vitu huwa vinaonekana tofauti ukivitazama katikati ya miguu yako ukiwa umeinama. (Source: CNN)

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles