ASHA BARAKA AMPIGIA MAGOTI RAIS MAGUFULI

0
1098

                                                                        

                                                                   |Scholastica Wilson, Dar es SalaamBendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ inatarajia kuadhimisha miaka 20 tangu kuanzishwa kwake.

Katika maadhimisho hayo bendi hiyo imeandaa tamasha kubwa la muziki wa dansi litakalofanyika 29 Septemba Ukumbi wa Club Legend (zamani Nyumbani Lounge).

Mkurugenzi wa bendi hiyo, Asha Baraka, amewaambia waandishi wa habari kwamba katika maadhimisho hayo bendi ya Twanga Pepeta itafanya shughuli mbalimbali za kijamii kama ishara ya kuwashukuru mashabiki zake.

“Tunakusudia kutembelea Hospitali ya Mwananyamala, tutatoa pia majaketi nakishi (Jacket reflectors) kwa madereva wa pikipiki, hii ni maalum kwa kumuenzi muimbaji wetu, Abdul Semwando aliyefariki kwa ajali ya pikipiki pia tutatembelea vituo kadhaa vya watoto yatima,” amesema Asha.

Mkurugenzi huyo pia ametuma maombi kwa Rais John Magufuli ili aruhusu wanamuziki wa dansi wapige muziki kama zamani zaidi ya saa sita usiku kwa kuwa muziki ndiyo ajira ya vijana wengi.

Naye kiongozi wa bendi, Luiza Mbutu amesema bendi hiyo imezuia baadhi ya waliokuwa wanamuziki wake kurudi katika bendi hiyo kwa kuwa wataua bendi walizopo.

Hata hivyo, Asha Baraka ametoa onyo kwa watu wanaoiba na kuweka nyimbo za bendi ya Twanga Pepeta kwenye mitandao yao bila ridhaa yao huku akionya pia wasanii  wanaocheza nyimbo zao mikoani  kwa kuwa wanakiuka sheria ya haki miliki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here