27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Asasi za kiraia zataka uchunguzi kifo mmiliki wa shule

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

BAADA ya taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kwamba marehemu Sheikh Rashid Bura (62),  kwamba alifariki  kwa ugonjwa wa shinikizo la damu, asasi za kirai nchini zimeliomba Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi huru na wa kina kuhusiana  na kifo hicho.

Hatua hiyo imekuja kufuatia marehemu Bura kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Dalai Islamic Centre,  ambayo ilikuwa moja ya asasi za kiraia iliyokuwa ikihudumia yatima na watoto wanaioshi katika mazingira magumu.

Marehemu Bura alikutwa Jumatano ofisini kwake Mtaa wa Kuu Street katika eneo la Majani ya Chai  mjini hapa akiwa amefariki  huku mazingira ya kifo chake yakiacha maswali mengi.

Mazingira  ya kifo cha marehemu Bura hadi sasa yamegubikwa na utata baada ya mwili wake kukutwa ukiwa haina nguo na majeraha kadhaa.

Wakizungumza na MTANZANIA jana viongozi wa asasi hizo walisema kuna haja ya kufanya uchunguzi wa kina juu ya kifo hicho kutokana na utata ambao unaendelea kujitokeza.

Mwenyekiti wa Mtandao wa Asasi za Kirai Jiji la Dodoma (Dungonet),  Manance Muhumpa alisema anaamini Jeshi la Polisi halitaishia lilipoishia na badala yake litafanya uchunguzi wa kina kuhusiana na kifo hicho.

“Jeshi letu la Polisi linafanya kazi kwa weledi na ninaamini uchunguzi haujaishia pale taarifa za kipelelezi lazima ziendelee ili tweze kujua na mashaka yetu yaweze kupotea,” alisema.

Alisema marehemu alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Dungonet na alikuwa na mchango mkubwa ambao hauwezi kusaulika.

“Alitufundisha weledi, alituunganisha Waislamu na Wakristo, jamii fukara za kati, hakuwa mtu mwenye majivuno, tumepoteza kiungo kikubwa sana sisi asasi za kiraia,” alisema.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na Masuala ya Wanawake (WOWAP) na Mbunge wa Viti Maalumu, Fatma Toufiq (CCM), alisema jamii inatakiwa kutokuwa na shaka kutokana na taarifa za daktari kuonesha kwamba amefariki kwa ugonjwa moyo.

Alisema daktari ndio mtu wa mwisho hivyo hakuna ambaye anatakiwa kuhoji taarifa hiyo.

“Nilifika eneo la tukio mapema kabisa niliona kila kitu, nilikuwa nasubiria taarifa ya Polisi na imeonesha kwamba amefariki kwa ugonjwa wa moyo huwezi tena kuhoji,”alisema.

Akimzungumzia marehemu alisema alikuwa na ushawishi mkubwa katika asasi za kirai ambapo alidai kwamba Tanzania imempoteza mpambanaji ambaye alikuwa tayari kuuza kila kitu chake kwa ajili ya yatima.

“Mwaka jana alienda Hijja na tiketi yake nilimpa mimi sababu ya mchango mkubwa ambao alikuwa akiutoa kwetu kwenye asasi za kiraia,fikra zake tutaendelea kuzibeba kusaidia mayatima,” alisema.

ALIKUWA AKISOMESHA WATOTO 97

Akizungumza na MTANZANIA jana mtoto wa marehemu, Sada Bura alisema kwamba baba yake alikuwa akisomesha zaidi ya watoto 95 katika shule ya Zamzam ambao walikuwa ni yatima na na wanaishi katika mazingira magumu.

KAMANDA AGEUKA MBOGO

Jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,  Gilles Muroto aligeuka mbogo mara baada ya mwandishi wa habari hii kumuuliza ni watu wangapi wanashikiliwa kutokana na tukio hilo.

Kamanda Muroto alihoji taarifa hizo zimepatikana wapi na hawezi kuzungumza kwa sababu tayari aliishatoa taarifa.

“Hizo habari umezipata wapi? nasema hivi hizo habari umezitoa wapi? waulize wao sisi hatuna habari, nimeishatoa taarifa juzi,” alisema Muroto

Juzi akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda Muroto alisema marehemu Bura alipatwa na mauti akiwa ofisini kwake kutokana na shinikizo la moyo, taarifa ambayo ilizua shaka huku wanafamilia wakiipinga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles