24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Asas yatoa msaada wa vifaa vya kujikinga na corona kwa waandishi wa habari

Raymond Minja

Kampuni ya usindikaji wa maziwa (Asas) ya mkoani Iringa imetoa msaada wa barakoa 1,000 kwa waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari vya jijini Dar es Salaam ili waweze kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona.

Akizungumzia msaada huo Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Kampuni hiyo, Ahmed Salim amesema wameamua kusaidia kundi hilo kutokana na mchango wake kwa jamii katika kipindi hiki hiki cha janga la corona.

Amesema kazi za waandishi wa habari zinawahitaji kukutana na watu mbalimbali hivyo wanapaswa kuwa na vifaa vya kujikinga na maambukizi hivyo kampuni hiyo inaamini imetoa msaada sehemu sahihi.

“Nyie ni watu muhimu katika kuhabarisha jamii kuhusu maambukizi ya corona hivyo ni imani yetu kuwa barakoa hizi 1,000 zitasaidia kwa muda na tutaendelea kushirikiana na Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo Habari Tanzania (JOWUTA) kusaidia hali ikiruhusu,” amesema.

Akizungumzia msaada huo Katibu Mkuu wa JOWUTA, Suleiman Msuya ameipongeza kampuni hiyo kwa kuwakumbuka waandishi wa habari wa Dar es Salaam ambao walikuwa wanapitia changamoto ya uhaba wa vifaa hivyo.

“Tunaishukuru Kampuni ya Asas kwa msaada huu wa Barakoa 1,000 zitatusaidia sana katika kipindi hiki kigumu naamini sasa tutafanya kazi kwa uhuru na hata tukiandika habari na makala za kusisitiza uvaaji barakoa tunaonekana kwa mfano,” alisema Msuya.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles