25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 21, 2023

Contact us: [email protected]

ASAP Rocky asitisha ziara za Julai

NEW YORK, MAREKANI

BAADA ya kukutwa na hatia ya kumshambulia shabiki wake nchini Sweden, rapa Rakim Mayers maarufu kwa jina la ASAP Rocky, ametangaza kusitisha ziara zake za muziki kwa kipindi hiki cha Julai kwa ajili ya kumaliza kesi yake.

Wiki moja iliopita msanii huyo alikuwa nchini Sweden kwa ajili ya tamasha la muziki, lakini siku moja kabla ya tamasha hilo msanii huyo alikamatwa na polisi baada ya kumsukuma shabiki yake hadi kuanguka kwa madai hakutaka kupiga naye picha.

Chanzo cha karibu na msanii huyo kimeweka wazi kuwa, Julai hii hatoweza kufanya chochote katika kazi zake za muziki hadi akimalizana na kesi yake ambayo inamkabili.

Hata hivyo, hadi sasa msanii huyo anashikiliwa na polisi nchini Sweden kutokana na tukio hilo. Mashabiki kwenye mitandao ya kijamii wameaza kupaza sauti zao kutaka mamlaka yatoe maamuzi ili msanii huyo aweze kuwa huru na kazi zake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles