29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Arteta afikiria nahodha mpya

LONDON, ENGLAND

KOCHA wa timu ya Arsenal, Mikel Arteta, ameweka wazi kuwa, kwenye kikosi chake kuna shida ya mchezaji kiongozi ndani na nje ya uwanja.


Mshambuliaji wa timu hiyo Pierre Aubameyang kwa sasa ndio wa nahodha wa timu hiyo akichukua nafasi ya Granit Xhaka tangu Oktoba mwaka jana baada ya mashabiki wa timu hiyo kumzomea wakidai hana mchango wowote na timu.


Wakati timu hiyo ipo chini ya kocha Unai Emery, alikuwa anabadilisha nahodha, hivyo jumla alitumia watano ambao ni Aubameyang, Xhaka, Hector Bellerin, Alexandre Lacazette na Mesut Ozil.


Lakini baada ya wachezaji kupiga kura mwanzoni mwa msimu huu jina la Xhaka likajitokeza sehemu nyingi kabla ya Aubameyang kuja kuchukua nafasi hiyo.


Kutokana na mwenendo wa timu hiyo, Arteta amedai timu hiyo inahitaji nahodha ambaye atakuwa anafanya majukumu yake ndani ya uwanja na kuleta mafanikio makubwa.


“Lazima tuwe na nahodha mwenye mchango mkubwa ndani ya kikosi, aweze kuwa na ushawishi kwa ajili ya timu, hata mashabiki wamekuwa wakihitaji nahodha wa namna hiyo.


“Kuna sababu nyingi za mchezaji kuwa nahodha, zingine zinakuwa ngumu kuzifikia, lakini kwa sasa ninaamini hakuna shida hiyo ya nahodha kwa kuwa mambo yanakwenda sawa, hivyo hakuna sababu ya kubadilisha nahodha wakati kuna mambo mengine mengi ya msingi ya kuyaangalia, ila ukifika wakati nitafanya maamuzi hayo.


“Nimewahi kuwa kwenye klabu ambayo ina manahodha watano. Hiyo inakuwa moja kati ya timu yenye viongozi wengi kuliko nahodha. Lakini mwisho wa siku mmoja ndiye ambaye anavaa kitambaa na wengine wanabaki kama wachezaji viongozi,” alisema kocha huyo.


Aliongeza kwa kusema, anaamini nahodha ana umuhimu mkubwa sana ndani ya kikosi, lakini muda bado haujafika wa kufanya mabadiliko, kitu cha msingi nahodha aliyopo kuhakikisha anatekeleza wajibu wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles